Dar Es Salaam,Tanzania.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),linapenda kuwatangazia wanafamilia wote wa mpira wa miguu wenye nia ya kuwania uongozi kuwa limewarahisishia namna ya kupata fomu baada ya tovuti ya TFF:www.tff.or.tz kuwa kwenye marekebisho.
Kwa wanafamilia ambao wapo nje ya Dar es Salaam, wanaotaka fomu hizo kwa sasa hawana budi kutuma ujumbe wa barua pepe kwenda kwenye anwani ya info@tff.or.tz na moja kwa moja atajibiwa kwa kupata fomu hizo ziliazoanza kutolewa leo Juni 16, mwaka huu. Kwa walioko Dar es Salaam, wanaweza kupata fomu hizo katika ofisi za TFF zilizo Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Mwanafamilia wa mpira wa miguu mwenye nia ya kugombea ataweza kufungua fomu hizn na kuzijaza huku akifuata utaratibu wa kulipia kwenye nambari ya akaunti 01J1019956700
katika Benki ya CRDB.
Zoezi hili kuchukua fomu na kuzirejesha fomu lililoanza leo Juni 16, litafikia kikomo Juni 20, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya 10.8 ya Uchaguzi kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya TFF.
Mara baada ya kulipia, Mgombea atawajibika kuwasilisha stakabadhi ya malipo kutoka
benki na kupewa fomu ya nafasi husika.
Gharama za kuchukulia fomu ni.
1. Rais TSHS 500,000/=
2. Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
3. Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS
200,000/=
0 comments:
Post a Comment