Rustenburg, Afrika Kusini
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars leo Jumanne itajitupa tena dimbani huko Meruleng Rustenburg nchini Afrika Kusini mishale ya 2:30 Usiku kucheza mchezo wake wa pili wa kundi A kwa kumenyana na Angola kuwania nafasi moja ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Cosafa Castle.
Taifa Stars inaingia kwenye mchezo wake wa leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wake wa kwanza kwa kuifunga Malawi mabao 2-0.Mabao yote yalifungwa na winga wake wa kushoto,Shiza Ramadhan Kichuya.Angola iliibamiza Ushelisheli bao 1-0 lililofungwa na Manguxi.
Ikiwa Taifa Stars itashinda mchezo wake wa leo itakuwa imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kubaki kileleni mwa msimamo wa kundi A kwa kuwa na wastani mzuri wa pointi za mabao ya kufunga.
Mchezo wa mapema leo utakoanza mishale ya saa 10:00 jioni utazikutanisha Malawi na Ushelisheli ambazo bado hazijaonja radha ya ushindi tangu michuano hiyo ilipoanza Jumapili iliyopita.
Taifa Stars itashuka tena dimbani Alhamisi ya wiki kucheza mchezo wake wa mwisho wa kundi A kwa kuvaana na Ushelisheli.Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Moruleng.Angola itacheza na Malawi.Mshindi wa kundi hili atacheza na wenyeji Afrika Kusini kwenye hatua ya robo fainali.
0 comments:
Post a Comment