Nice,Ufaransa.
MSHAMBULIAJI mtukutu wa Italia,Mario Balotelli amehitimisha ile sintofahamu ya wapi atakuwa msimu ujao baada ya Jumapili ya leo kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea klabu yake ya sasa ya OGC Nice ya Ufaransa.
Balotelli mwenye umri wa miaka 26 sasa ameamua kusalia OGC Nice licha ya kutakiwa na vilabu vya Borussia Dortmund ya Ujerumani na Besiktas ya Uturuki pamoja na vilabu vya Hispania na nyumbani kwao Italia.
Balotelli alijiunga na OGC Nice mwezi Agosti mwaka jana kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya £3.8m akiwa mchezaji huru baada ya kutupiwa virago na klabu yake ya Liverpool aliyojiunga nayo kwa ada ya £17m akitokea AC Milan.
Msimu uliopita Balotelli aliifungia OGC Nice mabao 17 katika michezo 28 na kuiwezesha klabu hiyo ya Allianz Riviera kukata tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao baada ya kushika nafasi ya tatu Ligue 1.
0 comments:
Post a Comment