Liverpool,England.
KLABU ya Liverpool imekamilisha usajili wa winga wa zamani wa Chelsea, Mohammed Salah kutoka AS Roma ya Italia kwa ada ya uhamisho ya £34.4m (Bilioni 8.5).
Salah,25,anayetokea Misri amesaini mkataba wa miaka mitano na kukabidhiwa jezi namba 11 ambayo awali ilikuwa inavaliwa na Roberto Firmino aliyepewa jezi namba 9.
Salah aliyekubali mshahara wa £90,000 kwa wiki anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Liverpool katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Mwingine ni Dominic Solanke aliyetokea Chelsea.
0 comments:
Post a Comment