Dar Es Salaam,Tanzania.
KLABU ya Yanga kupitia kwa Katibu wake Mkuu,Charles Mkwasa imekiri kushindwa vita ya kumbakiza kikosini kiungo wake mahiri ,Mnyarwanda Haruna Niyonzima.
Mkwasa amesema Yanga haitaweza kuwa na Niyonzima msimu ujao baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya na kiungo huyo aliyedumu Jangwani kwa kipindi cha misimu sita.
Mkwasa ameongeza kuwa wameamua kumwachia Niyonzima licha ya kwamba walikuwa bado wanamuhitaji kwa misimu miwili ijayo.
0 comments:
Post a Comment