Istanbul,Uturuki.
ALIYEKUWA mshambuliaji wa Swansea City,Mfaransa Bafetimbi Gomis ameihama klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki.
Gomis mwenye umri wa miaka 31 amejiunga na Galatasaray kwa kandarasi ya miaka mitatu baada ya kufaulu vipimo vyake vya afya jana mchana.
Swansea City inatarajiwa kupokea kitita cha £2.5m kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji huyo iliyemsajili mwaka 2014 akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake katika klabu ya Olympique Lyon ya Ufaransa.
Akiwa na Swansea City Gomis alifanikiwa kuifungia klabu hiyo ya Liberty Stadium mabao 17 katika michezo 71 huku shangilia yake ya mabao mfano wa dubu ikiwakosha mashabiki wengi.
Msimu uliopita Gomis aliichezea Marseille kwa mkopo wa msimu mmoja ambapo alifanikiwa kufunga mabao 20 katika michezo 31.
Gomis anakuwa mchezaji wa pili kuihama Swansea City katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Mwingine ni mlinzi wa zamani wa kushoto wa St Etienne,Franck Tabanou.
Swansea City inatarajiwa kuziba pengo la Gomis kwa kumsajili kwa mkopo wa msimu mmoja mshambuliaji kinda wa Chelsea na timu ya taifa ya England,Tammy Abraham
Msimu uliopita Abraham mwenye umri wa miaka 19 aliichezea klabu ya daraja la kwanza ya Bristol City na kufanikiwa kuifungia mabao 23.
0 comments:
Post a Comment