Nairobi, Kenya.
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ya Kenya imetangaza kuwa itasitisha udhamini kwa washirika wake wote ikiwemo vilabu vya soka vya nchi hiyo kuanzia Januari 1,2018.
Hilo limewekwa wazi leo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Ronald Karauri kupitia ujumbe aliouweka kwenye ukurasa wake wa twitter.
Uwamuzi huo umefikiwa baada ya hivi karibuni Serikali ya Kenya kuamua kuyakata kodi ya asilimia 35 makampuni yote yanayojishughulisha na michezo ya kubashiri.
Kusitisha udhamini kwa kampuni ya SportPesa kutakuwa ni pigo kwa vilabu vya Gor Mahia,AFC Leopards na Nakuru All Stars ambavyo vimekuwa vikiendesha shughuli za kila siku kwa kutegemea pesa kutoka kampuni hiyo.
Chama cha soka cha Kenya (Football Kenya Federation) pamoja bodi inayosimamia ligi kuu ya nchi hiyo (Kenya Premier League Board) ni washirika wengine ambao watasitishiwa udhamini na kampuni ya SportPesa.Vilabu vya Tanzania vya Simba,Yanga pamoja na Singida United vyenyewe vitaendelea kufaidi matunda ya udhamini kutoka kampuni hiyo.
0 comments:
Post a Comment