Kigali,Rwanda.
SINGIDA United imeendelea na mikakati yake ya kukiimarisha kikosi chake tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu bara baada ya jioni ya leo kumsajili mshambuliaji hatari wa Polisi ya Rwanda,Danny Usengimana.
Usengimana mwenye umri wa miaka 21 amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu baada ya kushuka daraja miaka 16 iliyopita.
Usengimana anayeichezea pia timu ya taifa ya Rwanda anaiacha Polisi akiwa ameifungi mabao 16 msimu uliopita ambapo aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya soka nchini Rwanda.
Msimu uliopita pia Usengimana aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 16 sawa na wa Muhadjiri Hakizimana wa Mukura ambaye kwasasa anaichezea APR.
0 comments:
Post a Comment