728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 19, 2017

    SAFI:Ally Mayay Tembele ajitosa kuwania Urais TFF


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    KIUNGO na nahodha wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania,Ally Mayay Tembele leo amejitosa kuwania nafasi ya kuliongoza shirikisho la soka nchini Tanzania,TFF baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais. 

    Ally akiwa amesindikwa na wachezaji wenzake wa zamani aliwasili kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume,Dar Es Salaam na kuchukua fomu hiyo tayari kuanza mapambano ya kumng'oa Rais wa sasa wa shirikisho hilo,Jamal Malinzi ambaye aliingia madarakani miaka minne iliyopita kuchukua nafasi ya Edgar Chilla Tenga aliyekuwa amemaliza muda wake wa uongozi.

    Mbali ya Ally mwingine aliyechukua fomu leo hii ni Mtemi Ramadhani ambaye pia ni mchezaji wa zamani.Mtemi yeye anagombea nafasi ya Makamu wa Rais.

    Uchaguzi mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu huko mkoani Dodoma.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAFI:Ally Mayay Tembele ajitosa kuwania Urais TFF Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top