Marseille,Ufaransa.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa,Valere Germain (Pichani) akiwa ameshikilia jezi ya Marseille mara baaada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na timu hiyo akitokea Monaco kwa ada ya usajili ambayo haijawekwa wazi.
Germain mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Marseille kwa mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vyake ya afya.
Msimu uliopita Germain aliifungia Monaco mabao 10 na kuiwezesha timu hiyo ya Stade Louis II kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Ligue 1 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000.
Germain anakuwa mchezaji wa pili kuihama Monaco katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wa kwanza alikuwa ni Mreno Bernardo Silva aliyejiunga na Manchester City kwa ada ya £43m.
0 comments:
Post a Comment