Paris,Ufaransa.
ARSENAL imeripotiwa kuwa imemfanya mshambuliaji wa Bordeaux,Gaetan Laborde kuwa chaguo lake la tatu ikiwa itashindwa kuwasajili washambuliaji wawili inaowasaka kwa udi na uvumba,Alexandre Lacazette wa Lyon na Kylian Mbappe wa Monaco.
Laborde mwenye umri wa miaka 23 anatazamwa na Arsenal kwa jicho la tatu baada ya msimu uliopita kufungia Bordeaux mabao 13 na kutoa pasi tano za mabao katika michezo 42.
Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinasema tayari Arsenal imeshawasiliana na Bordeaux kuulizia upatikani wa mshambuliaji wa zamani wa Stade Montois.
Arsenal imemgeukia Laborde baada ya kuanza kuingiwa na hofu ya kuwakosa Mbappe na Lacazette ambao licha ya kuuzwa kwa fedha nyingi pia wamekuwa wakisakwa na vilabu vingi vikubwa na vinavyojua kumwaga noti.
Mpaka sasa Arsenal imeshafanikiwa kufanya usajili mmoja peke yake tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya kwa kumsajili mlinzi wa kushoto wa Shalke 04 ya Ujerumani,Sead Kolasinac.
0 comments:
Post a Comment