728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 21, 2017

    OUT:New Zealand yatupwa nje kombe la mabara



    Kuban,Urusi.

    NEW ZEALAND imekuwa timu ya kwanza kutupwa nje ya michuano ya kombe la mabara baada ya usiku huu kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mexico katika mchezo wa pili wa kundi A uliochezwa kwenye uwanja wa Olimpiyskiy Stadion Fisht.

    New Zealand ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Chris Wood aliyefunga katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

    Kipindi cha pili kilishuhudia Mexico iliyokuwa imepumzisha wachezaji wake wanane wa kikosi cha kwanza ikija juu na kuanza kuwashambuliaji wapinzani wao New Zealand kama nyuki.

    Mashambilizi hayo yalizaa matunda baada ya Mexico kupata mabao mawili katika dakika za 54 na 72 kupitia kwa Raul Jimenez na Oribe Peralta baada ya kazi nzuri ya winga Javier Aquino aliyekuwa mwiba kwa mabeki wa New Zealand.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OUT:New Zealand yatupwa nje kombe la mabara Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top