London,England.
KLABU ya Arsenal leo Jumatano imetambulisha jezi zake za nyumbani za rangi nyekundu za msimu mpya wa 2017/18 itakazozitumia kwenye michuano ya ligi kuu ya soka nchini England pamoja na michuano mingine.
Jezi hizo ambazo zimetengenezwa na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Puma zitaanza kuuzwa Julai 3 mwaka huu kwenye maduka mbalimbali duniani kote.
Mbali ya kutambulisha jezi hizo pia Arsenal imeitumia siku ya leo kutambulisha mabadiliko kidogo yaliyofanyika hasa katika namba za jezi za wachezaji ambapo beki mpya wa klabu hiyo,Sead Kolasinac amepewa jezi namba 31 ambayo hapo awali ilikuwa ikivaliwa na kinda Mfaransa,Jeff Reine-Adelaide.
Aidha katika utambulisho huo jezi namba 7 ambayo imekuwa ikivaliwa na Alexis Sanchez imeonekana ikiwa na jina la mshambuliaji, Danny Welbeck mgongoni hali ambayo imeibua wasiwasi kuwa huenda staa huyo wa Chile akatimka klabuni hapo.
0 comments:
Post a Comment