Paul Manjale,Dar Es Salaam.
YANGA SC imezidi kuzitimulia vumbi Simba na Azam kwenye orodha ya ubora wa viwango vya soka kwa ngazi za vilabu barani Afrika.
Katika orodha iliyotolewa leo Jumanne na mtandao wa kimataifa wa footballdatabase.com maalumu kwa mwezi Aprili imeonyesha kuwa Yanga SC imeshika nafasi 337 baada ya kujikusanyia pointi 1252.
Azam imeshika nafasi ya 360 ikiwa imejikusanyia pointi 1249,Simba imeshika nafasi ya 365 baada ya kujikusanyia pointi 1247.Nafasi ya kwanza imeshikwa na Esperance de Tunis ya Tunisia.Nafasi ya pili na ya tatu imeshikwa na Al Ahly ya Misri na TP Mazembe ya Congo DR.
Vilabu vilivyofika nafasi 15 za juu iko kama ifuatavyo
1. Esperance de Tunis
2. Al Ahly
3. TP Mazembe
4. Etoile du Sahel
5. Vita Club
6. Al-Merreikh
7. Al Hilal Omdurman
8. Wydad Casablanca
9. Mamelodi Sundowns
10. El Zamalek
11. Kaizer Chiefs
12. CS Sfaxien
13. Dynamos
14. Raja Casablanca
15. Coton Sport
0 comments:
Post a Comment