728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 26, 2017

    Niyonzima,Migi waitwa Amavubi kuivutia kasi Jamhuri ya Afrika ya Kati


    Kigali,Rwanda.

    KIUNGO fundi wa Yanga SC na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kigeni wa ligi kuu bara, Haruna Niyonzima 'Fabregas' amejumuishwa kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 25 cha Rwanda (Amavubi) ambacho kimetajwa leo na kocha Antoine Hey tayari kwa mchezo wake wa Juni 11 wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON utakaochezwa huko Bangui dhidi ya wenyeji wao Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Mbali ya Niyonzima nyota wengine waliopata bahati ya kujumuishwa kwenye kikosi cha Amavubi kutoka nje ya ardhi ya Rwanda ni pamoja na Jean Baptiste Mugiraneza 'Migi' na Jacques Tuyisenge wa Gor Mahia ya Kenya.

    Wengine ni Salomon Nirisarike wa AFC Tubize,Emery Bayisenge wa KAC Kénitra,Fitina Omborenga, Jean Claude Iranzi na Rachid Kalisa wa MFK Topvar Topoľčany ya Slovakia pamoja na Ernest Sugira wa AS Vita ya Congo DR.

    Kikosi Kamili

    Makipa :Eric Ndayishimiye (Rayon Sports), Marcel Nzarora (Police Fc) na Olivier Kwizera (Bugesera Fc)

    Mabeki : Aimable Rucogoza (Bugesera),Salomon Nirisarike (AFC Tubize), Aimable Nsabimana (APR Fc), Thieryy Manzi (Rayon Sports), Emery Bayisenge (KAC Kénitra),Fitina Omborenga (MFK Topvar Topoľčany),Michel Rusheshangoga (APR Fc), Emmanuel Imanishimwe (APR FC) and Eric Iradukunda
    (AS Kigali)

    Viungo :Ally Niyonzima (Mukura VS),Olivier Sefu Niyonzima (Rayon Sports), Jean Baptiste Mugiraneza (Gor Mahia), Djihad Bizimana (APR Fc), Jean Claude Iranzi (MFK Topvar Topoľčany ),Dominique Savio Nshuti (Rayon Sports), Haruna Niyonzima (Young Africans), Rachid Kalisa (MFK Topvar Topoľčany)

    Washambuliaji :Jacques Tuyisenge (Gor Mahia),Danny Usengimana (Police Fc), Gilbert Mugisha (Pepiniere), Ernest Sugira (As Vita Club) and Justin Mico (Police Fc)
      
    Rwanda ambayo iko kundi H pamoja na mataifa ya Cote d'Ivoire,Guinea na Jamhuri ya Afrika ya Kati imepania kufuzu michuano ya AFCON kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 2004 katika michuano iliyofanyika nchini Tunisia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Niyonzima,Migi waitwa Amavubi kuivutia kasi Jamhuri ya Afrika ya Kati Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top