728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 27, 2017

    Arsenal yabeba mwali wa FA,yaigonga Chelsea 2-1 Wembley


    London,Engand.

    ARSENAL imetwaa ubingwa wake wa tatu wa kombe la FA baada ya usiku huu kuifunga Chelsea mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley jijini London.

    Mabao yaliyoipa Arsenal ubingwa huo yamefunga na Alexis Sanchez aliyefunga bao la kwanza.Bao la pili limefungwa na Aaron Ramsey kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Olivier Giroud aliyekuwa ameingia uwanja sekunde chake akitokea benchi.



    Bao la Chelsea limefungwa na Diego Costa kwa mkwaju wa karibu baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Willian.Aidha katika mchezo huo Chelsea ililazimika kumaliza ikiwa pungufu baada ya winga wake Victor Moses kutolewa uwanjani kwa kadi mbili za njano kwa kosa la kujidodosha.


    Ushindi huo umeifanya Arsenal iwe ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa FA.Jumla imetwaa mara 13.Ikifuatiwa na Manchester United iliyotwaa mara 12.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Arsenal yabeba mwali wa FA,yaigonga Chelsea 2-1 Wembley Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top