728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 31, 2017

    Dortmund,Psg zakubaliana ada ya Pierre-Emerick Aubameyang


    Paris,Ufaransa.

    KLABU ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani imekubali dau la £61m kutoka klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake mahiri Pierre-Emerick Aubameyang.

    Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo Sport France ni kwamba Aubameyang ambaye ni mfungaji bora wa Bundesliga wa msimu uliopita amekubali mkataba wa miaka mitano na atakuwa akilipwa mshahara wa £168,000 kwa wiki.

    Yahoo Sport France imeendelea kuripoti kuwa Aubameyang anayetokea nchini Gabon pia atavuna kitita cha £5.25m kama ada binafsi ya usajili.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Dortmund,Psg zakubaliana ada ya Pierre-Emerick Aubameyang Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top