728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 24, 2017

    AFCON U-17:Ghana yaibutua Niger na kutangulia fainali


    Libreville, Gabon.

    TIMU ya taifa ya vijana ya Ghana ya chini ya umri wa miaka 17,Black Starlets imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya AFCON ya vijana ya U-17 baada ya jioni ya leo kuwafunga vijana wenzao wa Niger kwa penati 6-5 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa huko Port Gentil.

    Mpaka dakika tisini zinaisha hakuna timu iliyokuwa imepata bao licha ya kushambuliana kwa zamu.

    Penati za Ghana zimefungwa na Terry Owusu,Gideon Acquah,Faisal Osman,Ibrahim Sulley,Emmanuel Toku na Mohamed Idriss huku penati ya nahodha Eric Ayiah ikipanguliwa na kipa wa Niger,Khaled Lawal aliyekuwa nyota wa mchezo.

    Mchezo mwingine wa nusu fainali utachezwa hapo baadae ambapo mabingwa watetezi Mali watacheza na Guinea.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AFCON U-17:Ghana yaibutua Niger na kutangulia fainali Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top