728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 23, 2017

    Arsenal yajiingiza mbio za kumtaka mfungaji bora ligi kuu nchini Ubelgiji



    London,England.

    ARSENAL imeripotiwa kutia miguu na kujiingiza mazima kwenye mbio za kumwania mfungaji bora wa ligi kuu ya nchini Ubelgiji Mnigeria,Henry Onyekuru anayechezea klabu ya KAS Eupen.

    Taarifa za ndani zinasema tayari Arsenal imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wa winga huyo kampuni ya Uwakala ya Mercato Sports.

    Onyekuru mwenye umri wa miaka 19 ameibuka kuwa bidhaa inayosakwa kwa nguvu barani Ulaya baada ya msimu huu kuifungia klabu yake KAS Eupen mabao 25 na kusaidia upatikanaji wa mengine 14 hali iliyofanya aibuke mfungaji bora wa ligi kuu ya nchini Ubelgiji msimu wa 2016/17.

    Onyekuru anayedaiwa kuwa na kipendele kinachomruhusu kuuzwa kwa £6.8m ameripotiwa kuvutiwa zaidi na mpango wa kujiunga na Arsenal kwa madai kuwa ni klabu yenye nafasi kubwa moyoni mwake na angependa afuate nyayo za shujaa wake Mfaransa,Thierry Henry aliyepata mafanikio klabuni hapo.

    Hata hivyo Arsenal italazimika kupambana vilivyo ili kuhakikisha inainasa saini ya nyota huyo kwani vilabu vya Borussia Monchengladbach,Celtic,Club Brugge,Everton, Southampton na West Brom navyo vimeonyesha nia ya kumtaka Onyekuru.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Arsenal yajiingiza mbio za kumtaka mfungaji bora ligi kuu nchini Ubelgiji Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top