728x90 AdSpace

Saturday, May 27, 2017

Watford yapata kocha wa tisa katika kipindi cha miaka mitano


Watford,England.

WATFORD imemtangaza kocha wa zamani wa Hull City Mreno,Marco Silva kuwa kocha wake mkuu mpya.

Silva mwenye umri wa miaka 39 amesaini mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Walter Mazzarri aliyefutwa kazi.

Silva anakuwa kocha wa tisa kujiunga na Watford katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kocha wa nane tangu timu hiyo ianze kumilikiwa na familia ya Pozzo mwaka 2012.

Kabla ya kutua Watford,Silva aliwahi kuzifundisha timu za Sporting Lisbon na Olympiacos kabla ya mwezi Januari kujiunga na Hull City ambayo hivi karibuni imeshuka daraja.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Watford yapata kocha wa tisa katika kipindi cha miaka mitano Rating: 5 Reviewed By: Unknown