728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 27, 2017

    Hizi hapa tetesi za usajili kuwahusu:James,Pepe,Morata,Silva,nk

    JAMES:James Rodriguez anataka kuihama Real Madrid na kujiunga Manchester United badala ya Inter Milan ambayo iko tayari kutoa dau nono ili kuinasa saini yake.Limeripoti Diariogol.

    Inter Milan iko tayari kutoa €60m ili kumnasa nyota huyo raia wa Colombia dau ambalo ni kubwa kuliko lile la Manchester United la €40m.

    James amekaririwa akisema kuwa yupo tayari kubaki Real Madrid kwa msimu mmoja zaidi kama uhamisho wake kwenda Manchester United utakwama.


    GIANLUIGI:Taarifa kutoka nchini Italia zinasema AC Milan imemwambia kipa wake namba moja Gianluigi
    Donnarumma pamoja na wakala wake Mino Raiola kuwa iwapo hawatakaa mezani na kusaini mkataba mpya basi kipa huyo mwenye umri wa miaka 18 ataozea benchi.Limeandika La Gazzetta dello Sport.

    Gianluigi bado ana mkataba na AC Milan mpaka 2018.Ameahidiwa kitita cha €3.5m kama atasaini mkataba mpya na kubaki AC Milan.


    PEPE:Newcastle United inataka kuiongezea makali safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili mshambuliaji mahiri wa Angers ya Ufaransa,Muivory Coast,Nicolas Pepe.

    Pepe,22,ameanza kuwindwa na vilabu vingi Ulaya hasa baada ya kuisaidia Angers kutinga fainali ya kombe la ligi la Ufaransa (French Cup) ambapo leo Jumamosi itavaana na Paris Saint-Germain.

    Mbali ya Newcastle United vilabu vya Monaco,Olympique Marseille na Wolfsburg pia vimeripotiwa kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye thamani ya £8m.


    MORATA:Manchester United imedaiwa kuwa itapunguza bei ya kipa wake,David de Gea kutoka €75m mpaka kufikia €25m ikiwa Real Madrid itakubali kumjumuisha Alvaro Morata kwenye dili la la kumnasa kipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid.


    MOURA.Kocha wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho ana matumaini ya kusajili winga wa kulia msimu huu na tayari jicho lake limeshatua kwa winga wa Paris Saint-Germain,Lucas Moura.Limeripoti SportWitness.

    Mourinho ameamua kumgeukia Moura baada ya kugundua kuwa atakumbana na upinzani mkali katika mpango wake wa kutaka kumsajili Willian kutoka Chelsea.


    SILVA:Watford imefungua mazungumzo na kocha wa zamani wa Hull City,Mreno Marco Silva kwa ajili ya kuchukua nafasi ya kocha wake wa sasa Walter Mazzarri limeripoti Daily Mirror.

    Silva anaelekea kubakia ligi kuu England baada ya uhimisho wake kwenda Porto kukwama.Crystal Palace pia inamtaka kocha huyo ili achukue nafasi ya Sam
    Allardyce aliyejiuzulu mapema wiki hii.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hizi hapa tetesi za usajili kuwahusu:James,Pepe,Morata,Silva,nk Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top