Faridi Miraji,Dar Es Salaam.
Timu ya Simba Sc ilipeleka malalamiko kwenye shirikisho la Soka duniani FIFA kulalamika maamuzi ya kamati ya katiba, Sheria hadhi za wachezaji kubatirisha maamuzi ya Ile kamati ya masaa 72 iliyoipa Simba pointi tatu kutoka kagera sugar kutokana na Simba kumlalamikia Mohamed Fakhi akicheza mechi dhidi ya Simba wakidai ana kadi tatu za njano.
Barua ya fifa kwenda Simba kupitia Kwa shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inasema kutokana na sheria za FIFA maamuzi yaliyofikiwa na shirikisho la Soka kwenye nchi husika , Fifa haina uwezo wa kutoa maamuzi mengine zaidi. Na hivyo maamuzi yaliyofikiwa na kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji ya TFF yanabaki kama yalivyo
0 comments:
Post a Comment