Manchester,England.
Manchester City imekamilisha usajili wa kiungo Mreno ,Bernardo Silva kutoka AS Monaco ya Ufaransa.
Silva mwenye umri wa miaka 22 amejiunga na Manchester City kwa ada ya uhamisho ya £43m na amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea miamba hiyo ya Etihad.
Silva ambaye atakuwa akivalia jezi namba 20 anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Pep Guardiola ambaye amepania kufanya usajili wa kufa mtu msimu ujao baada ya Manchester City kushindwa kutwaa taji lolote msimu huu.
Tayari Guardiola ameshawaonyesha mlango wa kutokea wakongwe Pablo Zabaleta, Jesus Navas,Willy Caballero, Gael Clichy pamoja na Bacary Sagna ili kuzipisha damu changa kikosini.
0 comments:
Post a Comment