Dodoma,Tanzania.
Kocha Joseph Omog wa Simba amesema ubigwa wa Kombe la FA waliupata jana utairudisha timu hiyo kwenye ushindani kama ilivyokuwa zamani.
Omog ambaye hilo ni taji lake la kwanza tangu aanze kuifundisha Simba msimu
huu amesema sasa anajisikia amani pengine kuliko mtu yeyote kwenye benchi la ufundi.
"Niwapongeze wachezaji na viongozi pia kwa kuweza kufanikisha kile ambacho
tulikuwa tunakihitaji mchezo ulikuwa mgumu lakini ubingwa huu unatufanya
tuwe bora zaidi msimu ujao kwenye michuno yote tutakayoshiriki," amesema
Omog.
Mcameroon huyo amesema kazi yake kubwa sasa ni kujenga kikosi cha msimu ujao ambacho kitaweza kutetea ubingwa wao lakini pia kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Amesema angependa kuona Simba inafika mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kama alivyofanya kwa AC Leoards ya Congo Brazaville.
Amesema mchezo wa juzi hatousahau baada ya wapinzania wao Mbao kuwapa wakati mgumu hasa baada ya kusawazisha bao dakika za mwisho.
Simba itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika 2018 wakati Yanga ambao ndiyo mabingwa wa ligi ya Vodacom watashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
0 comments:
Post a Comment