Rio De Janeiro,Brazil.
STAA wa Barcelona,Neymar hajajumuishwa kwenye kikosi cha Brazil ambacho mwezi ujao kitasafiri kwenda nchini Australia kwa ajili ya kucheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki ya kujipima nguvu.
Kocha mkuu wa Brazil,Tite amesema ameamua kutomjumuisha kikosini staa huyo ili kumpa muda wa kutosha wa kupumzika ili akusanye nguvu za kufanya kwenye kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika nchini Urusi.
Wengine walioachwa kikosini ni mabeki Marquinhos wa Paris - Saint Germain na Daniel Alves wa Juventus.Staa wa Liverpool,Philippe Coutinho pamoja na staa wa Manchester City,Gabriel Jesus wao wameendelea kuwemo kikosini.
Ikiwa nchini Australia,Brazil itashuka dimbani Juni 9 kuvaana na Argentina kabla ya siku nne baadae kucheza na wenyeji wao Australia.Michezo yote itachezwa kwenye jiji la Melbourne.
Kikosi Kamili
Makipa:Diego Alves (Valencia), Weverton (Atletico-PR), Ederson (Benfica)
Mabeki:David Luiz (Chelsea), Gil (Shandong Luneng), Jemerson (AS Monaco),Rodrigo Caio (Sao Paulo), Thiago Silva (PSG), Alex Sandro (Juventus), Fagner (Corinthians), Filipe Luis (Atletico Madrid),Rafinha (Bayern Munich)
Viungo:Fernandinho (Manchester City),Giuliano (Zenit), Lucas Lima (Santos),Paulinho (Guangzhou Evergrande), Philippe Coutinho (Liverpool), Renato Augusto (Beijing Guoan), Rodriguinho (Corinthians), Willian (Chelsea)
Washambuliaji:Diego Souza (Atletico-PR), Douglas Costa (Bayern Munich), Gabriel Jesus (Manchester City), Taison (Shakhtar Donetsk)
0 comments:
Post a Comment