728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 24, 2017

    Msuva,Tshabalala,Manula watamba usiku wa tuzo ligi kuu bara

    Simon Msuva mfungaji bora ligi kuu bara


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    HAFLA ya kukabidhi tuzo kwa wachezaji,makocha,waamuzi na timu zilizofanya vizuri ligi kuu bara msimu wa 2026/17 zimefanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City uliopo maeneoya Survey jijini Dar Es Salaam.

    Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,Dk Harrison Mwakyembe ilishuhudiwa Tuzo ya Mchezaji bora wa msimu ikienda kwa beki wa kushoto wa Simba SC na timu ya Taifa,Mohammed Hussein Tshabalala akiwashinda Simon Msuva wa Yanga,Haruna Niyonzima wa Yanga,Aishi Manula wa Azam FC na Shiza Kichuya wa Simba. 


    Mwamuzi bora Elly Sasii

    Tuzo ya Mfungaji bora imekwenda kwa Simon Msuva wa Yanga na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting waliofungana baada ya wote kufunga mabao 14 kila mmoja.

    Tuzo ya Kipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Azam FC aliyeibuka mshindi baada ya kuwashinda Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Owen Chaima wa Mbeya City.Tuzo ya Mwamuzi bora imekwenda kwa Elly Sasii wa Dar Es Salaam akiwashinda Shomari Lawi wa Kigoma na Hance Mabena wa Tanga.



    Tuzo ya Kocha bora imekwenda kwa Mecky Mexime wa Kagera Sugar akiwazidi Joseph Omog wa Simba na Ettiene Ndayiragije wa Mbao FC.Tuzo ya mchezaji bora chipukizi imekwenda kwa Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar aliyewashinda Mohammed Issa wa Mtibwa Sugar na Shabani Iddi wa Azam FC.

    Tuzo ya Mchezaji bora wa kigeni imekwenda kwa Haruna Niyonzima wa Yanga huku tuzo ya bao bora la msimu ikienda kwa Shiza Kichuya wa Simba.Ni lile bao alilolifunga dhidi ya Yanga katika ushindi wa mabao 2-1.Amejinyakulia kita cha shilingi millioni tatu (3).Kikosi Bora cha Wachezaji wa Ligi Kuu wa msimu ni; Aishi Manula (Azam), Salum Kimenya (Prisons), Mohammed Hussein (Simba), Yakoub Mohammed (Azam FC), Method Mwanjali (Simba), Kenny Ally (Mbeya City), Simon Msuva (Yanga), Haruna Niyonzima (Yanga), Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting) na Shiza Kichuya (Simba).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Msuva,Tshabalala,Manula watamba usiku wa tuzo ligi kuu bara Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top