Paul Manjale,Dar Es Salaam.
PAZIA la ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL linatarajiwa kufungwa leo Jumamosi kwa timu zote 16 za ligi hiyo michezo minane ya ligi hiyo kushuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu huku timu mbili zikitarajiwa kuungana na JKT Ruvu kushuka daraja mpaka daraja la kwanza FDL.
Mabingwa watarajiwa wa ligi hiyo,Yanga SC watakuwa ugenini CCM Kirumba,Mwanza kucheza na wenyeji wao Mbao FC ambao wamepania kushinda mchezo huo ili wakwepe mkasi wa kushuka daraja.
Timu nyingine zinazopambana kukwepa kushuka daraja ni pamoja na Ndanda FC ya Mtwara ambayo leo itakuwa nyumbani Nangwanda Sijaona kucheza na JKT Ruvu ambayo tayari imeshashuka daraja.
Toto Africans itakuwa na kibarua kigumu cha kuitafuna miwa ya Mtibwa Sugar pale itakapokuwa ugenini Manungu Complex,Morogoro Kujaribu kuvuna pointi tatu muhimu.Michezo yote itachezwa saa 10:00 jioni ili kuwepa upangaji wa matokeo.
Ratiba Kamili
Mbao FC vs Yanga SC
Simba SC vs Mwadui FC
Azam FC vs Kagera Sugar
Majimaji vs Mbeya City
Stand United vs Ruvu Shooting
Tanzania Prisons vs African Lyon
Mtibwa Sugar vs Toto African Ndanda FC vs JKT Ruvu
0 comments:
Post a Comment