Dar Es Salaam,Tanzania.
Katika kuelekea mchezo wa fainali ya FA utakaofanyika tare27 mwezi huu mjini Dodoma,shirikisho la kandanda Tanzania TFF limeanika wazi viingilio vya mchezo huo huku likiweka utaratibu wa namna ya kujiandikisha na namna ya kupata tiketi kwa wapenzi wa soka za kuwawezesha kutazama mtanange huo.
Kwa mujibu wa TFF imeelezwa kua "wapenzi wa mpira wa miguu wanaweza kujiandishisha kwenye ofsisi za vyama vya mpira wa miguu vya mikoa waliyopo kulingana na aina ya tiketi wanayohitaji ili wapatiwe tiketi hiyo pindi watakapofika dodoma".
Mwisho wa watu kujiandikisha itakua ni siku ya jumatano ya tarehe 24/05/2017 na baada ya hapo tiketi zitapatikana Dodoma siku ya ijumaa tarehe 26/05/2017 na jumamosi pale uwanja wa Jamuhuri Dodoma.
Hata hivyo katika mchezo huo viingilio vita kua katika mgawanyo ufuatao:-
VIP A - 20,000/- ( WATU,500)
VIP B - 15,000/-(WATU 1500)
MZUNGUKO - 5000/-(WATU 20,000)
0 comments:
Post a Comment