728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 26, 2017

    Ziara ya Everton Tanzania yawiva,kuja na jeshi lake kamili


    Liverpool,England.

    KLABU ya Everton yenye makao yake makuu kwenye jiji la Liverpool,England itakuwa timu ya kwanza kutoka nchini humo kuja kuzuru Tanzania pale itakaposhuka kwenye uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam kucheza mchezo mmoja wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017/18 ikiwa ni sehemu ya kusherekea udhamini walioupata kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportpesa.

    Taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu hiyo iliyoshika nafasi ya saba kwenye ligi kuu ya England iliyoisha wiki iliyopita,imesema Everton itashuka kwenye Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 kucheza na mshindi wa michuano mipya ya SportPesa Super Cup Alhamisi ya Juni 13.

    Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Juni 5 hadi 11 jijini Dar es Salaam,ikishirikisha timu za Simba SC, Yanga SC, Singida United na Jang'ombe Boys za Tanzania.Gor Mahia,AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC za Kenya.

    Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia zawadi ya kitita cha Dola 60,000 pamoja na kupata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Everton ambayo itakuja na nyota wake wote akiwemo mshambuliaji wake mahiri,Romelu Lukaku.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ziara ya Everton Tanzania yawiva,kuja na jeshi lake kamili Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top