728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 24, 2017

    Jamani Defoe anakwenda kupiga pesa ndefu Bournemouth


    London,England.

    MSHAMBULIAJI wa Uingereza,Jermain Defoe atajiunga na Bournemouth hivi karibuni akiwa mchezaji huru baada ya kuchomoa kubakia kwenye kikosi cha Sunderland ambacho kimeshuka daraja msimu huu.

    Defoe mwenye umri wa miaka 34 ameripotiwa kuwa atajiunga na Bournemouth kwa mkataba wa miaka mitatu ambao utamwingizia kiasi cha Pauni 20 Milioni za Kiingereza.

    Defoe amedaiwa kuwa ametengua kipengele kilichokuwa kwenye mkataba wake na Sunderland na atajiunga na Bournemouth ambayo aliwahi kuichezea zamani wakati anaanza kucheza soka la ushindani.

    Defoe alikuwa na miaka 18 wakati anajiunga na Bournemouth kwa mara ya kwanza mwaka 2000-01 akitokea West Ham United kwa mkopo na kufanikiwa kufunga mabao 19 katika michezo 31 aliyoichezea timu hiyo ya jiji la London. 

    Akiwa Bournemouth,Defoe alifanikiwa kucheza pamoja na Eddie Howe na Jason Tindall ambao kwa sasa ni makocha wakuu na wasaidizi wa timu hiyo.

    Defoe alijiunga na Sunderland Januari 2015 akitokea Toronto FC ya Canada kwa sharti kwamba ataruhusiwa kuihama timu hiyo bure iwapo itashuka daraja.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Jamani Defoe anakwenda kupiga pesa ndefu Bournemouth Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top