728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 25, 2017

    Azam FC yathibitisha kuachana na John Bocco


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati,Azam FC jioni ya leo wamethibitisha kuachana rasmi na Mshambuliaji wao ambaye pia ni Nahodha wao,John Raphael Bocco maarufu kama Adebayor.

    Akithibitishwa hilo Afisa Habari wa timu hiyo,Jaffari Iddi Maganga amesema ni kweli wameachana na Bocco na rasmi kuanzia sasa mchezaji huyo si mali ya Azam FC.

    Maganga ameongeza kuwa wameachana na Bocco baada ya mshambuliaji huyo mrefu aliyehudumu kwa zaidi ya miaka kumi (10) kumaliza mkataba wake klabuni hapo.

    Ameongeza pia kuwa Azam FC inamtakia Bocco maisha mema kokote kule atakakoamua kwenda iwe ndani au nje ya nchi.

    Kauli hiyo ya Azam FC imekuja huku kukiwa na taarifa kuwa tayari Bocco ameshasaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba SC kwa dau la Shilingi Milioni 48.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Azam FC yathibitisha kuachana na John Bocco Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top