Libreville,Gabon.
WAFUNGAJI bora wa ligi kuu bara msimu huu,Simon Msuva wa Yanga na Abrahman Mussa wa Ruvu Shooting watapewa zawadi sawa baada ya wote kuibuka vinara baada ya kufunga mabao 14.Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Malinzi ameandika "Kwa kuwa vijana wetu Abrahman Mussa na Simon Msuva wamefungana mabao 14.Wote ni wafungaji bora watapewa zawadi sawa ya @Tsh5.8m.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa ligi kuu bara kushuhudiwa tuzo/zawadi ya mfungaji bora ikienda kwa wachezaji wawili.
0 comments:
Post a Comment