London,England.
EDEN Hazard pichani akiwa na tuzo yake baada ya kutangazwa mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea katika hafla ya kutunuku tuzo iliyofanyika Jumapili usiku huko Battersea Evolution,London akiwashinda Cesar Azpilicueta,David Luiz na N’Golo Kante.
Katika hafla hiyo iliyoendeshwa na Mtangazani Jeremy Vine pamoja na Mchekeshaji Omid Djalili pia ilishuhudiwa Hazard akitwaa tuzo ya pili usiku huo baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya bao bora la mwaka.Bao hilo ni lile alilofunga dhidi ya Arsenal.
N’Golo Kante ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka chaguo la wachezaji.Ikumbukwe Kante ndiye mchezaji bora wa mwaka ligi kuu England.Nahodha John Terry ametwaa tuzo ya heshima.
Wengine waliotwaa tuzo:Karen Carney ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka.Tuzo ya mchezaji bora wa Akademi imekwenda kwa Mason Mount.
0 comments:
Post a Comment