London,England
MLINZI wa kimaifa wa Argentina,Pablo Zabaleta (Pichani) akitia saini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na West Ham United.
Zabaleta mwenye umri wa miaka 32 amejiunga na West Ham United baada ya klabu yake ya sasa ya Manchester City kugoma kumpa mkataba mpya yeye pamoja na wachezaji wengine watano wenye umri mkubwa.
Mlinzi huyo wa zamani wa Espanyol ya Hispania anaiacha Manchester City akiwa ameichezea jumla ya michezo 300.
0 comments:
Post a Comment