728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 29, 2017

    Wakenya waifuata saini ya kipa wa Mbao FC


    Dodoma,Tanzania.

    KLABU ya Sony Sugar inayoshiriki Ligi Kuu Kenya, imeingia vitani na timu za Bongo kuwania saini ya kipa wa timu ya Mbao FC,Benedict Haule, baada ya kuvutiwa na kiwango chake.

    Sony Sugar imeonyesha nia ya kumsajili kipa huyo na tayari mazungumzo ya awali yamefanyika lakini kuna klabu nyingine za Ligi Kuu Bara zimeanza kumnyemelea.

    Haule alisajiliwa na Mbao katika dirisha dogo msimu huu, akitokea Panone FC
    inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ndiye aliyedakia timu yake katika mechi zote za FA walipokutana na Yanga na Simba ikiwamo ya fainali juzi.

    Kipa huyo amesema baada ya kumalizikia kwa ligi huenda asiendelee kuichezea klabu kwa kuwa anahitajiwa na timu ya Sony Sugar na nyingine za Tanzania.

    Alisema tayari wameshafanya mazungumzo ya awali na klabu hiyo na walikuwa wanasubiri Ligi Kuu Bara ifikie ukongoni ili wamalizane.

    “Licha ya kuwa kuna timu nyingine za hapa nyumbani zinanihitaji na viongozi wake wameanza kunipigia simu, naipa kipaumbele Sony Sugar kwa sababu malengo yangu ni kucheza nje ya nchi ila nitaangalia na makubaliano na dau lao litakavyokuwa,”alisema.

    Alisema wakati wa mapumziko ya mzunguko wa kwanza ikiwa ndio amesajiliwa na Mbao,walienda kucheza mechi ya kirafiki na klabu hiyo ndipo wakavutiwa naye kumwambia baada ya ligi wanamhitaji.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wakenya waifuata saini ya kipa wa Mbao FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top