Milan,Italia.
GENNARO Gattuso (Kushoto) akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya vijana ya AC Milan.
Gattuso mwenye umri wa miaka 39 amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa Primavera na kutanabaisha kuwa kukubali kwake kukinoa kikosi cha vijana cha AC Milan hakumaanishi kuwa amepiga hatua kurudi nyuma kwani alikuwa tayari ameshahudumu kama kocha mkuu katika vilabu vya wakubwa vya Sion,Palermo, OFI Crete na Pisa
Katika enzi za uchezaji wake Gattuso aliiwezesha AC Milan kutwaa makombe mawili ya Serie A na makombe mawili ya klabu bingwa Ulaya katika kipindi cha miaka 13 alichohudumu katika klabu hiyo ya San Siro.
0 comments:
Post a Comment