728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 26, 2017

    Waamuzi wa Fainali ya ASFC hadharani



    Kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya michuano ya Azam Sports Federation Cup HD msimu wa 2016/17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Ahmed Kikumbo wa Dodoma kuwa mwamuzi wa mchezo wa fainali kati ya Simba SC na Mbao SC utakaofanyika Uwanja wa Jamburi Mei 27, 2017 kuanzia saa 10.00 jioni.

    Kikumbo atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon pia wa Dodoma wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Peter Temu wa Arusha. 

    TFF inazitakia timu zote, Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na Kamishna wao pamoja na wanafamilia wa mpira wa miguu, mchezo mzuri wenye fanaka kwa kila upande.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Waamuzi wa Fainali ya ASFC hadharani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top