728x90 AdSpace

Wednesday, May 24, 2017

SportsPesa yaja na michuano mipya,Simba,Yanga,Singida kugombea Milioni 60


Faridi Miraji,Dar Es Salaam.

SportsPesa wamezindua rasmi mashindano Kwa washirika wake Katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki , mashindano haya yatajulikana kwa Jina la  SportPesa Super Cup'

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika nchini Tanzania kwa kuzishirikisha timu za Simba, Yanga , Jang'ombe na Singida United  zote kutika Tanzania. Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars (Hizi zote toka nchini Kenya)

Bingwa wa SportPesa Super Cup ataondoka na kitita cha dola 30,000 (60m) huku mshindi wa pili akipata dola 10,000 (20m).

Mashindano haya  yanatarajiwa  Kutimua Vumbi kuanzia Juni 5 na kufika tamati Juni 11.

Ratiba 

5-June 
Singida United vs FC Leopard
Yanga vs  Tusker FC

6-June 

Simba Vs Nakuru All Star
Jang`ombe boys vs Gor mahia

Nusu fainali tarehe 8-June 
-Mshindi 01 VS mshindi 02
-Mshindi 03 VS mshindi 04

Fainali ni tarehe 11-June. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: SportsPesa yaja na michuano mipya,Simba,Yanga,Singida kugombea Milioni 60 Rating: 5 Reviewed By: Unknown