KEANE:Jose Mourinho ameitaka bodi ya Manchester United hasa mtendaji wake mkuu Ed Woodward kufanya haraka awezavyo ili kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati wa Michael Keane kama hajaporwa na vilabu vingine.Limeripoti Daily Mail.
Keane mwenye thamani ya £24m amedaiwa pia kuwaniwa na Liverpool ambayo imemfanya kuwa chaguo lake la pili baada ya mlinzi wa Southampton,Virgil van Dijk.
GOMEZ:Mario Gomez amedokeza kuwa atakuwa tayari kuihama Wolfsburg ikiwa klabu hiyo itashuka daraja msimu huu.Limeripoti Bild.
Gomez mwenye miaka 31 ana kipengele kinachomruhusu kuondoka Wolfsburg kwa €10 na amesema atahama ikiwa klabu hiyo itafungwa na Eintracht Braunschweig kwenye mchezo wa mtoano wa kuwania tiketi ya kubaki Bundesliga.
PERISIC:Manchester United imeanza mazungumzo na Inter Milan ili kuangalia uwezekano wa kumsajili winga wake wa kushoto Ivan Perisic.Limeripoti Daily Mail.
Hivi karibuni Perisic mwenye miaka 28 amekuwa akihusishwa na mpango wa kutaka kuondoka San Siro na kwenda kusaka changamoto kwingine.
Inter Milan imeripotiwa kuwa tayari kumuuza ili kwa ajili ya kutunisha pesa zaidi za kufanyia usajili.
LEMAR:Juventus imemweka juu kabisa ya orodha ya wachezaji inaowataka winga wa Monaco,Mfaransa Thomas Lemar.Limeripoti L'Equipe.
Juventus inamtaka winga huyo wa zamani wa Caen ili aisaidie kuimarisha upande wake wa kushoto na iko tayari kutoa €30 ili kuinasa saini yake.
BARKLEY:West Ham imeripotiwa kuwa iko tayari kupambana na Tottenham katika vita ya kumwania kiungo wa Everton,Ross Barkley.Limeripoti Daily Star.
Kocha wa West Ham,Slaven Bilic yuko tayari kutoa mshahara wa £140,000 kwa wiki ili kumnasa kiungo huyo wa Kiingereza.
NEYMAR:Barcelona imeripotiwa kuwa tayari kumtumia Neymar kama sehemu ya dili la kumnasa kiungo wa Paris Saint-Germain,Marco Verratti.Yahoo imeripoti.
Taarifa zinadai Paris Saint-Germain bado haijatoa jibu juu ya pendekezo hilo la Barcelona licha ya hapo awali kudaiwa kuwa iliwahi kufanya mazungumzo na wakala wa Neymar.
SILVA:Lionel Messi amedaiwa kusikitishwa na kitendo cha Barcelona kushindwa kumsajili kiungo wa Monaco,Bernardo Silva ambaye juzi alitimkia Manchester City kwa ada ya £43m.Limeripoti Don Balon.
ROONEY:Majaaliwa ya Wayne Rooney kutaka kurejea kwenye klabu yake ya utotoni ya Everton yameanza kukumbana na vigingi baada ya uongozi kudaiwa kugawanyika.Limeripoti The Sun.
Taarifa za ndani zinasema baadhi ya viongozi wa Everton hawataki Rooney arejee Goodson Park na badala yake wanataka aletwe mshambuliaji mwingine mwenye umri mdogo.
0 comments:
Post a Comment