Paul Manjale,Dar Es Salaam.
ALIYEKUWA mfungaji bora wa michuano ya Kombe la FA msimu uliopita,Atupelee Green amejiunga na wageni ligi kuu bara,Singida United akitokea JKT Ruvu ya Pwani.
Taarifa rasmi zinasema Atupelee amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na JKT Ruvu ambayo imeshuka daraja na msimu ujao itacheza ligi daraja la kwanza.
Atupelee anakuwa mchezaji wa pili mzawa kujiunga na Singida United baada ya Kenny Ally Mwambungu aliyejiunga wiki iliyopita akitokea Mbeya City ya mkoani Mbeya.
Kabla ya kutua Singida United,Atupele pia aliwahi kuchezea Coastal Union,Yanga,Kagera Sugar na Ndanda FC ya Mtwara.
0 comments:
Post a Comment