728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 29, 2017

    Huddersfield Town yapanda ligi kuu baada ya miaka 45


    London,England.

    Huddersfield Town imepanda kucheza ligi kuu ya soka nchini England baada ya leo jioni kuifunga Reading kwa penati 4-3 katika mchezo mgumu uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley.

    Huddersfield Town na Reading zililazimika kupigiana penati ili kumpata mshindi baada ya kushindwa kufungana ndani ya dakika 120.

    Huddersfield Town inakuwa timu ya tatu kupanda ligi kuu msimu huu baada ya Newcastle United na Brighton & Holve.

    Mara ya mwisho timu hiyo West Yorkshire kucheza ligi kuu ilikuwa ni mwaka 1972.Miaka 45 iliyopita.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Huddersfield Town yapanda ligi kuu baada ya miaka 45 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top