Lubumbashi,Congo.
KAMPUNI ya kutengeneza vinywaji vikali ya Simba Breweries ya nchini DR Congo imesaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi wa kuendelea kuwadhamini mabingwa watetezi wa ligi kuu ya nchini hiyo,TP Mazembe.
Mkataba huo mpya ambao haujawekwa wazi thamani yake umedaiwa kuwa pia utawawezesha wachezaji wa TP Mazembe kuvuna mamilioni ya pesa kama bonasi kwa kila mchezo mmoja watakaokuwa wanashinda kwenye michuano ya Afrika.
"Wachezaji watakuwa wanapata bonasi kutoka kwa wadhamini wetu,Simba Breweries kwa kila mchezo watakaokuwa wanashinda kwenye michuano ya Afrika.Amesema Fredric Kitengie,Mkurugenzi wa Michezo wa TP Mazembe.
Pia mkataba huo mpya utaipa haki nembo ya Simba Breweries kuendelea kuweka makazi kwenye jezi zote za TP Mazembe pamoja na mbao zote za matangazo zilizomo ndani ya uwanja wa klabu hiyo yenye mafanikio zaidi nchini DR Congo.
0 comments:
Post a Comment