Barcelona,Hispania.
HATIMAYE Barcelona leo imemtangaza kocha wa zamani wa Athletic Bilbao,Ernesto Valverde kuwa Kocha wake mkuu mpya.
Valverde,53,maarufu kama El Txingurri amekubali mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza kujiweka pembeni baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu.
Kabla ya kujiunga na Athletic Bilbao,Valverde aliwahi kuvinoa vilabu vya Espanyol, Olympiacos, Villarreal pamoja na Valencia.
Valverde aliwahi kuichezea Barcelona kwa kipindi cha miaka miwili kati ya 1988 na 1990.Wakati huo Barcelona ilikuwa ikinolewa na Mholanzi,Johan Cruyff.
Valverde atatambulishwa mbele ya waandishi wa habari siku ya Alhamisi na kuwa kocha wa 56 wa Barcelona.
0 comments:
Post a Comment