728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 25, 2017

    Singida United yamnasa nahodha wa Mbeya City


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    SINGIDA United imeendelea na zoezi lake kabambe la kukisuka upya kikosi chake tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu bara baada ya hii leo kumsajili Kenny Ally Mwambungu kutoka Mbeya City ya jijini Mbeya na kumpa jezi namba 8.

    Kenny Ally anayecheza nafasi ya kiungo amesaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na Singida United ambayo imerejea ligi kuu msimu huu baada ya kushuka daraja miaka 16 iliyopita.




    Kiungo huyo ambaye pia alikuwa nahodha Mbeya City hapo awali alikuwa akiwaniwa na timu za Simba,Yanga na Azam FC anakuwa mchezaji wa kwanza mzawa kujiunga na Singida United.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Singida United yamnasa nahodha wa Mbeya City Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top