728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 29, 2017

    MABINGWA:Mali yatwaa tena AFCON U-17


    Libreville,Gabon

    MALI imefanikiwa kuutetea ubingwa wake wa michuano ya vijana ya Afrika (U-17) baada ya Jumapili usiku kuifunga Ghana bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Stade de Amitie huko Libreville,Gabon.

    Mali ambayo ilibaki kidogo isishiriki michuano hiyo baada ya mapema mwaka huu kufungiwa na FIFA kufuatia serikali yao kuingilia masuala ya mpira kabla ya kuruhusiwa katika dakika za mwisho,walionekana kiibana vyema Ghana ambayo ilikuwa moto wa kuotea mbali kwenye hatua ya makundi.

    Mamadou Samake ndiye aliyekuwa shujaa kwa upande wa Mali baada ya kufunga bao pekee na la ushindi katika dakika ya 22 ya kipindi cha kwanza akiuwahi mpira wa penati uliotemwa na kipa wa Ghana,Danlad Ibrahim aliyekuwa shujaa baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penati.

    Ushindi huo umeifanya Mali itwae ubingwa wa vijana wa Afrika mara mbili sawa na Ghana, Nigeria na Gambia .


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MABINGWA:Mali yatwaa tena AFCON U-17 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top