728x90 AdSpace

Wednesday, May 31, 2017

Singida United yachomoa mmoja Toto Africans



Dar Es Salaam,Tanzania.

SINGIDA United imeendelea kufanya kweli katika ujenzi wa kikosi chake tayari kwa kwa msimu mpya wa ligi kuu bara msimu ujao hii ni baada ya kufanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Toto Africans ya Mwanza,Salumu Chuku.

Chuku aliyeng'ara msimu uliopita licha ya Toto Africans kushuka daraja amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo inayonolewa na Mholanzi Hans Van Pluijm.

Chuku anakuwa mchezaji wa tatu mzawa kujiunga na Singida United.Wengine ni Kenny Ally Mwambungu aliyetokea Mbeya City na Atupele Green aliyetokea JKT Ruvu ya Pwani.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Singida United yachomoa mmoja Toto Africans Rating: 5 Reviewed By: Unknown