728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 31, 2017

    MAPEMA TU:Arsenal yamnasa mfungaji bora Ubelgiji,mshahara wa Shilingi Milioni 95 kwa wiki wamvuta Emirates


    Brussels, Ubelgiji.

    MABINGWA wa kombe la FA nchini England,Arsenal wamekubali kutoa ada ya uhamisho ya £6.8m kwa ajili ya kumsajili mfungaji bora wa ligi kuu ya soka nchini Ubelgiji,Henry Onyekuru anayekipiga katika klabu ya KAS Eupen.

    Taarifa kutoka mtandao wa Sky Sports zinasema Arsenal na KAS Eupen zimeshafikia makubaliano ya kuuziana nyota huyo mzaliwa wa Nigeria na zoezi la upimaji wa afya yake litafanyika Juni 12 mwaka huu.

    Onyekuru mwenye umri wa miaka 19 amekubali mkataba wa miaka mitano Arsenal na atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni 38,000 (Tsh 95,000,000) kwa wiki.


    Msimu huu Onyekuru ambaye ni zao la shule ya soka ya Aspire Academy aliibika mfungaji bora ligi kuu nchini Ubelgiji baada kufunga mabao 25 hali iliyofanya virabu vingi vikubwa barani Ulaya vianze kumfukuzia.

    Mbali ya Arsenal vilabu vingine ambavyo pia vimeonyesha nia ya kumsajili Onyekuru ni pamoja na Club Brugge,Anderlecht,Southampton, Everton,Celtic na Liverpool.

    Onyekuru anakuwa mchezaji wa pili kuripotiwa kuwa mbioni kutua Arsenal baada ya mlinzi wa kushoto wa Shalke 04 ya Ujerumani,Sead Kolasinic ambaye tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya na kufaulu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAPEMA TU:Arsenal yamnasa mfungaji bora Ubelgiji,mshahara wa Shilingi Milioni 95 kwa wiki wamvuta Emirates Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top