728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 30, 2017

    MKWARA:Mavugo simhofii mshambuliaji yeyote mpya


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MSHAMBULIAJI wa Simba, Laudit Mavugo,amesema hahofii ujio wa mshambuliaji yeyote mpya katika kikosi hicho.

    Kauli ya Mavugo imekuja baada ya kuwapo taarifa kwamba aliyekuwa mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco, amejiunga na Wekundu hao kwa ajili ya kuwachezea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

    Mavugo amesema yeye kama mchezaji siku zote amekuwa akihitaji changamoto mpya ili kumfanya kuwa bora zaidi.

    “Aje yeyote mimi ni profesheno, hivyo siwezi kumwogopa mchezaji mwenzangu, yeyote atakayesajiliwa mimi nitampa ushirikiano kwa kuwa lengo ni kuhakikisha Simba inafanya vizuri.

    “Mafanikio ya Simba ndio kitu muhimu mengine yanafuata,” alisema Mavugo.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MKWARA:Mavugo simhofii mshambuliaji yeyote mpya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top