Chiki Mchoma
Ha ha ha ha haaaaaa... 🤣🤣🤣
Leo nimeona nianze na kicheko kirefu.
Kuna watu kila kitu wao wanaona ni ndoto au ni siasa tu za mpira na sio uhalisia.
Hawaamini, hawajiamini, hawataki, wananuna, Roho zao zimejaa kwa nn..??
Wapo walionipigia simu eti kwa nini namfagilia Malinzi wakati si mtu wa Mpira na amefanya blanda kibao na TFF yake inaongoza kwa kusemwa Vibaya.
Wapo pia waliotuma meseji kulaumu na wengine kusema nimetumwa Kufanya Kampeni za Urais wa TFF.
Duuh... Mimi mtu mdogo sana na wala sina ushawishi wala mvuto wa kuwalisha sumu Wajumbe eti wampigie Kura Malinzi kwanza fitna za Soka naziwezea wapi??..
Na hata ikitokea hakushinda wala hainizuii kuendelea kumtaja Malinzi kama Mmoja wa Viongozi wa Kupigiwa mfano katika Soka la Tanzania.
Hao watu wa mpira wamekaa pale miaka na Miaka hakuna lolote la maana walilolifanya zaidi ya kuzidi kulipotezea misingi Soka letu.
Hata wachache waliotaka kujaribu kusimamia aidha walikosa uthabiti au walizidiwa na mbinu za walafi na kujikuta wanayumba kimaamuzi.
Soka halina Maajabu zaidi ya Uinuaji wa Soka la Vijana kitaalam na hilo ndilo linalonikosha kwa Rais Malinzi.
Soka letu lilipofikia lilihitaji mtu Mwenye Maono na Maamuzi Magumu kama aliyonayo Rais Malinzi na Sio kuwa Mwanasoka au Mtu wa Mpira tu. FULL STOP.
Na wengine wanaojiita watu wa Mpira ukiwafuatilia utakuta wapo pale TFF miaka na miaka wakifanya jukumu hili au lile lakini hawakuwahi kuwaza hata siku moja juu ya umuhimu wa TFF kutoa Ajira zaidi ya laki moja kama ambavyo leo hii Rais Malinzi anaziandaa kwa kujua au kwa kutokujua lakini mimi naziona na nina hakika atazifikia au hata akiondoka leo basi atakuwa ameacha Msingi imara wa Ajira hizo na atakayekalia kiti kile atajifanya kuwa ni sehemu ya Ajenda zake... Ajue wazi tushajua ni mipango thabiti ya Rais Malinzi awepo au asiwepo.
Ajira Zaidi Ya 50,000 Za Rais Malinzi.
Ni wazi kwa jinsi anavyoonesha Rais Malinzi anahitaji sana kukuza na kuendeleza Soka la Vijana.
Hakuna shaka wote tunajua kuwa vijana wengi wanapatikana Mashuleni na huko ndiko kuliko na Chimbuko la Wachezaji wengi waliowahi kuvuma nchi hii.
Shule zetu zina Walimu wa Michezo ambao hupata Taaluma hiyo kwenye vyuo vya ualimu katika kiwango cha mitaala ya ualimu na sio Elimu ya Soka ( Football Coaching Course ).
Kozi za Ualimu wa Soka ni Kozi Maalum na Msimamizi wa Kozi hizi ni TFF kupitia Vyama vya Soka Wilaya au Mkoa.
Sasa Basi!!
Tanzania bara pekee ina Shule za Msingi zisizopungua elfu 15. ( Kwa Makadirio ya Chini ).
Na shule za Sekondari zisizopungua Elfu Tatu. ( Kwa Makadirio ya Chini )
Achana na Shule binafsi na Vyuo vya Serikali na Vile vya Binafsi.
Ushaelewa Maana Yake??
Maana yake ni kuwa, kwa mpango ulio wazi wa Rais Malinzi juu ya Kuinua na kuendeleza Soka la Vijana nchini, ipo haja ya Shule zote hizi za Msingi na Sekondari kuwa na 'Qualified Coaches' ambao ni nje ya wale Waalimu wa Mitaala kule Mashuleni ili kupata 'Waalimu' sahihi zaidi wa Soka la Vijana.
Haya umeelewa hapo??
Iwapo shule hizo zote zitakuwa na 'Waalimu Wanataaluma wa Mpira wa Vijana' ni wazi kuwa tayari kutakuwa na Ajira kwa Makocha zaidi ya 18,000 nchi nzima.
Chukua pia Makocha wasaidizi 18,000 nchi nzima.
Usisahau mpira unapochezwa lazima kuwe na Madaktari wa Kusimamia na kuboresha afya za Wachezaji.
Kila shule ikipata Daktari Mmoja wa Michezo Maana yake tayari Kuna Ajira zingine zaidi ya 18,000 nchi nzima.
Narudia tena hapo haujaongelea suala la Vyuo na Shule Binafsi na Hiyo ni hesabu ya Makadirio ya Chini.
Huu ni Mpango wa lazima kama tunataka kuendeleza jitihada za Rais Malinzi ili kupata Vijana wenye Elimu toshelevu ya Soka la Utotoni ambalo ndilo Msingi wa Mafanikio ya Soka popote Duniani.
Wengi tunaamini Vipaji vya Wanasoka wetu wengi vilionekana tangu wakiwa Shuleni.
Kwenye Meza ya Rais Malinzi naona dhahiri jinsi Vipaji hivi vitakavyopelekewa Taaluma halisi ya Soka Mashuleni.
Ikifikia hatua hii, mimi binafsi naiomba Serikali ipokee Mawazo haya yenye Nia Njema.
Ajira zaidi ya 50,000 Mezani Kwa Rais Malinzi Inawezekana !!
Makocha, Madaktari wa Michezo tunazisubiri kwako Rais Malinzi.
0 comments:
Post a Comment