Munich,Ujerumani.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Gabon,Pierre-Emerick Aubameyang amekuwa Mwafrika wa pili kutwaa tuzo ya mfuk wa ligi ya Bundesliga "kicker Torjägerkanone" baada ya jioni ya leo kuifungia klabu yake ya Borussia Dortmund mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Werder Bremen katika mchezo wa mwisho wa kufunga msimu.
Mabao hayo mawili yamemfanya Aubameyang mwenye umri wa miaka 27 afikishe mabao 31 na kumpiku kwa tofauti ya bao moja mshambuliaji wa Bayern Munich,Robert Lewandowski aliyefunga mabao 30 msimu huu.
Nafasi ya tatu imeshikwa na mshambuliaji wa Cologne,Anthony Modeste aliyefunga mabao 25.Timo Werner wa RB Leipzig ameshika nafasi ya nne baada ya kufunga mabao 21.
Mwafrika wa kwanza kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi ya Bundesliga alikuwa ni Mghana,Tony Yeboah aliyetwaa tuzo hiyo mara mbili mfululizo msimu wa 1992-93 na 1993-94 akiwa na klabu ya Eintracht Frankfurt.
0 comments:
Post a Comment